Huwasilisha ujumbe kuhusu binadamu kuhusu utamaduni na uchumi.
Huwa na umbo mahsusi k.m. hadithi huwa na mwanzo, kati na mwisho na mashairi huwa na beti, mishororo, n.k.
Hutumia lugha kwa ufundi k.v. ya kitamathali.
Husawiri mandhari/mazingira mahsusi kwa ufundi mkubwa.
Hujenga wahusika kwa ustadi mkuu ili kusawiri tabia za watu katika jamii.
Tofauti Kati ya Fasihi na Sanaa Nyingine
fasihi
sanaa nyingine
ü Kutumia lugha
ü Sanaa tendi
ü Kutumia wahusika kuwasilisha maudhui
ü Kutumia maudhui na fani kuwasilisha ujumbe
ü Kujikita katika mazingira na wakati maalum
ü Kutotumia lugha
ü Si tendi
ü Hutumia maumbo kumithilisha watu
ü Kutumia maumbo na sura za vitu
ü Hazijikiti katika muktadha na wakati maalum.
Aina/makundi ya fasihi
Fasihi simulizi
Fasihi inayowasiolishwa kwa njia ya mdomo.
Fasihi andishi
Fasihi inayowasilishwa kwa njia ya maandishi.
Tofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi/sifa za fasihi simulizi/zinazofanya utanzu uwe wa fasihi simulizi
Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo ilhali fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi.
Fasihi simulizi huhifadhiwa akilini ilhali fasihi aandishi huhifadhiwa kwa maandishi.
Fasihi simulizi ni mali ya jamii ilhali fasihi andishi ni mali ya mtu binafsi/mwandishi.
Fasihi simulizi ina wahusika wa kila aina k.v binadamu, wanyama na ndege, mazimwi na majitu, miungu, mizimu, mashetani na vitu visivyo na uhai k.v. mawe na miti ilhali fasihi andishi ina wahusika binadamu kwa kiasi kikubwa.
Fasihi simulizi ina tanzu nyingi kuliko fasihi andishi.
Uwasilishaji wa fasihi simulizi huweza kuandamana na utendaji k.v matumizi ya ishara, nyimbo, makofi, kuimba, kubeba zana katika majigambo n.k ilhali ule wa fasihi andishi hauandamani na utendaji isipokuwa inapowasilishwa mbele ya hadhira.
Fasihi simulizi huwasilishwa mbele ya hadhira ilhali fasihi andishi si lazima iwasilishwe mbele ya hadhira.
Fasihi simulizi huwasilishwa mahali maalum k.v jandoni, matangani, arusini, n.k ilhali fasihi andishi haina mahali maalum.
Fasihi simulizi huandamana na shughuli fulani ya kitamaduni ilhali fasihi andishi haiandamani na shughuli ya kitamaduni.
Fasihi andishi huhitaji muda kutunga ilhali baadhi ya fasihi simulizi huzuka papo hapo k.m. semi, maigambo.
Fasihi simulizi ina uwezo mkubwa wa kubadilishwa na fanani anapowasilisha ufaraguzi) bali fasihi andishi haibadiliki isipokuwa mwandishi aiandike upya.
Fasihi simulizi ina historia ndefu kuliko fasihi andishi kwa kuwepo tangu mwanzo wa maisha ya binadamu
Fasihi simulizi huwasilishwa wakati maalum k.v. usiku, kipindi fulani cha mwaka ilhali andishi haina wakati maalum.
Tofauti kati ya hadhira
Hadhira ya fasihi simulizi huweza kuwasiliana moja kwa moja na mwasilishaji ilhali ile ya fasihi simulizi sio lazima iwasiliane na mwandishi.
Hadhira huchangia katika uwasilishaji wa fasihi simulizi k.v kwa kuimba, kupiga makofi n.k (hadhira tendi/hai) ilhali hadhira ya fasihi andishi haichangii katika uandishi.
Hadhira ya fasihi simulizi huonana na mwasilishaji ilhali ile ya fasihi andishi si lazima ionane na mwandishi.
Hadhira ya fasihi simulizi ni kubwa kuliko ile ya fasihi andishi kwani huhusisha hata wasiojua kusoma na kuandika.
Hadhira ya fasihi simulizi ni hai yaani inajulikana na fanani ilhali ile ya fasihi simulizi si hai yaani haijulikani na mwandishi.
Hadhira ya fasihi simulizi hainunui kazi ilhali ile ya fasihi andishi hununua kazi.
Hadhira ya fasihi simulizi yaweza kumiliki kazi ya fanani lakini ile ya fasihi andishi haiwezi kumiliki kazi ya mwandishi.
Hadhira ya fasihi simulizi huchagua kwa kulenga watu wa rika fulani lakini ile ya fasihi andishi hailengi watu wa rika yoyote.
Jinsi Fasihi Simulizi na Andishi Zinavyofanana
Zote mbili hushughulikia masuala yanayohusu maisha maisha ya binadamu.
Zote mbili Huhumia lugha kwa ubunifu kuwasilisha maudhui.
Zote mbili huwa na vipengele viwili vikuu, maudhui na fani (jumla ya mbinu msanii alizotumia kuwasilisha maudhui).
Zote mbili majukumu sawa k.v. kuburudisha, kuadilisha, kuhifadhi na kuendeleza utamaduni, n.k.
Zote mbili zina utendaji-pale tamthilia na riwaya zinapoigizwa.
Zote mbili huzaliwa, hukua na hufa kutegemea mabadiliko ya wakati.
Zote mbili huwa na wawasilishaji-fanani k.m. mtambaji/mganaji au manju/yeli katika fasihi simulizi na mwandishi upande wa fasihi andishi .
Majukumu ya Fasihi Simulizi/Umuhimu wa Kufunza Fasihi Simulizi Katika Shule za Upili
Kuburudisha-kustarehesha, kufurahisha, kuchangamsha, kutuliza, kusisimua na kupumbaza akili na kiwiliwili – nyimbo, hadithi, vitendawili
Kufunza maadili kwa wanajamii kwa kuwahimiza kuiga sifa chanya na kukataa sifa hasi za wahusika.
Kukuza uwezo wa kufikiri/kudadisi k.m vitendawili na chemshabongo.
Kufariji k.m mbolezi na methali k.m. ‘Baada ya dhiki faraja’.
Vipengele vya fasihi simulizi k.v mashairi, nyimbo, nahau, hutumiwa katika uandishi wa fasihi andishi.
Kuhifadhi historia ya jamii k.m. mighani, visaviini, mapisi, tarihi n.k.
Kukejeli tabia zinazokiuka matarajio ya jamii k.v soga, methali, n.k.
Kuendeleza tamaduni za jamii kwani husawiri imani na desturi za jamii. k.v kitendawili ‘Nyumbani mwetu mna papai lililoiva lakini siwezi kulichuma.’ – Mtu hawezi kumwoa dadake.
Kuunganisha watu pamoja kwa kuwajumuisha pamoja wakati wa ngoma, kuimba, utambaji, n.k.
Kukuza lugha k.v. misimu inapokita kimatumizi na kujumuishwa katika lugha sanifu.
Kukuza uwezo wa kutumia lugha kadiri mtu anapoendelea kuwasilisha k.v. hotuba, vitanza ndimi husaidia kuboresha matamshi na kutofautisha maana za maneno.
Kuza uwezo wa kubuni k.v. malumano ya utani, vitanza, ndimi ngonjera, n.k.
Kukuza uzalendo kwa kufanya wanajamii kuonea fahari jamii zao na kuiga mashujaa au watu waliotendea jamii makuu.
Kuonya na kutahadharisha wanajamii dhidi ya tabia hasi k.v. ulafi, uchoyo, n.k.
Sababu za Ufaraguzi/Kubadilika kwa Fasihi Simulizi
Kuwasilishwa vibaya.
Fanani kusahau na kubadilisha yaliyomo na mtiririko.
Kubadilisha ili kukidhi mahitaji ya hadhira k.m. umri na uelewa wao- kutumia lugha nyepesi kwa watoto na pevu kwa watu wazima.
Mabadiliko ya mandhari/mazingira-vitu vilivyo katika mazingira halisi kukosekana katika mazingira ya usimulizi na msimulizi kutumia vitu katika mazingira yake vinavyokaribiana navyo.
Kutoeleweka na hivyo kuhifadhiwa vibaya.
Mabadiliko ya wakati k.m kitendawili cha wakati wa mkoloni kutumia mzungu na cha wakati wa mwarabu kutumia mwarabu na maana ni ile ile-Mzungu/mwarabu amesimama kwa mguu mmoja-mwavuli.
Mabadiliko ya falsafa ya vizazi na maingiliano katika jamii kusababisha kurithisha tu yale ambayo ni muhimu na kuacha mengine.
Kila fanani huwa na mtindo wake wa kuwasilisha/kisanii.
Ubunifu wa fanani ili uwasilishaji uweze kuvutia saidi na uwezo wake wa lugha.
Teknolojia kusababisha kuhifadhiwa na hivyo kuiua.
Wahusika katika Fasihi Simulizi
Wahusika ni viumbe wa sanaa ambao hutumiwa katika kazi ya fasihi kuwasilisha maswala mbalimbali.
Fanani-anayetunga na kuwasilisha fasihi simulizi.
Hadhira-kusikiliza, kutazama, kushiriki wa kuimba, kuuliza maswali, kutegua vitendawili, kupiga makofi, n.k. kuna aina mbili za hadhira: (i) hadhira tendi/hai na (ii) hadhira tuli.
Wanyama-wanaofanya kama binadamu na kuwakilisha sifa kama vile ujanja, ulaghai, tamaa na ujinga na wanaobakia wanyama tu.
Binadamu
Mazimwi na majitu-viumbe vyenye matendo na maumbile ya kutisha kama vile jicho moja, vichwa viwili au zaidi, nusu mtu na nusu myama, wenye tamaa iliyokithiri ya kuweza kumeza kila kitu, kuhifadhi na kutunza binadamu ananyoyapendeza.
Wahusika vitu (visivyo na uhai) mawe, miti, vijaluba, vibuyu-hutumiwa kuibua imani za kidini.
Mizimu-roho za waliokufa-hutembea, hula na huathiri binadamu.
Miungu-viumbe vyenye uwezo mkubwa dhidi ya binadamu k.m. katika mighani na visasili.
Njia za Kukusanya Fasihi Simulizi
Kuchunza/utazamaji
Kutazama kwa makini yanayotokea na kuandika.
Umuhimu/ubora/uzuri
Kupata habari za kutegemewa na kuaminika.
Ni rahisi kurekodi k.v. kwa vinasa sauti, video, n.k.
Ni njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika
Kuweza kupata sifa za uwasilishaji k.v. toni/kiimbo, ishara n.k.
Kuweza kupata hisia halisi za uwasilishaji
Udhaifu
Shida ya mawasiliano.
Ugeni wa mtafiti kusababisha washiriki kumshuku na kusitisha uwasilishaji
Ghali kwa kumbidi mtafiti kusafiri
huhitaji muda mrefu
Kusikiliza wasanii wakiwasilisha tungo zao.
Umuhimu
Kuweza kupata sifa za uwasilishaji k.v. toni/kiimbo, ishara n.k.
Kupata habari za kutegemewa na kuaminika.
Ni rahisi kurekodi k.v. kwa vinasa sauti, video, n.k.
Kikwazo cha mawasiliano-Si njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika.
Kuweza kupata hisia halisi za uwasilishaji.
Udhaifu
Shida ya mawasiliano-Si njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika.
Huhitaji muda mrefu-kusafiri na kusikiliza.
Ugeni wa mtafiti kusababisha washiriki kutowasilisha ipasavyo.
Ghali kwa gharama ya usafiri.
Mahojiano
Kuhoji wanaofahamu mengi kuhusu fasihi simulizi.
Umuhimu
Kuweza kung’amua wakati mhojiwa anatoa habari zisizo za kweli.
Kuweza kufafanulia mhojiwa maswali ili kuweza kupata habari sahihi zaidi.
Kuweza kupata sifa za uwasilishaji k.v. toni/kiimbo, ishara n.k.
Ni rahisi kurekodi k.v. kwa vinasa sauti, video, n.k.
Kupata habari za kutegewa na kuaminika
Udhaifu
Huhitaji muda mrefu.
Mhojiwa kutotoa habari kwa kutomwamini mtafiti kwa ugeni wake.
Kikwazo cha mawasiliano-si njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika.
Ghali kwa gharama ya usafiri.
Kurekodi katika kanda za sauti/tepurekoda
Umuhimu
Kuweza kudumu na kufikia vizazi vingi.
Sifa za uwasilishaji/uhai kama vile toni na kiimbo kuhifadhiwa.
Mkusunyanyaji aweza kurudia uwasilishaji ikiwa hakuelewa.
Kupata habari za kutegewa na kuaminika
Kuweza kupata hisia halisi za uwasilishaji
Udhaifu
Chaweza kukosa nguvu za umeme na utafiti kuathirika.
Ghali kwa gharama ya ya usafiri na kununua filamu na kamera ya video.
Data yaweza kufisidiwa na hivyo kutowafikia walengwa.
f) Kupiga picha kwa kamera
Hunasa picha zisizo na miondoko na sauti
Umuhimu
Huonyesha uhalisi wa mandhari.
Huweza kuhifadhi ishara.
Mkusunyanyaji aweza kurudia uwasilishaji ikiwa hakuelewa.
Kupata habari za kuaminiwa na kutegemeka.
Udhaifu
Ghali kwa gharama ya ya usafiri na kununua kamera.
Sifa za uhai kama vile kiimbo haziwezi kuhifadhiwa.
Yaweza kukosa nguvu za umeme na utafiti kuathirika.
Data yaweza kufisidiwa na hivyo kutowafikia walengwa
Kushiriki katika kazi ya fasihi simulizi k.v. ngoma, soga, n.k.
Umuhimu
Kuweza kupata hisia halisi za uwasilishaji.
Kupata habari za kutegewa na kuaminika.
Njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika.
Kukuza utangamano wa mtafiti na wanajamii.
Kuweza kunasa na kuhifadhi sifa za kiimbo, toni na ishara.
Udhaifu
Kuchukua muda mrefu.
Ugeni wa msanii kusababisha washiriki kuwa na wasiwasi na kutotenda kama kawaida.
Njia ghali kwa kuhitaji mtafiti kusafiri mbali.
Mtafiti aweza kusahau kwa kuhifadhi akilini.
Kutumia hojaji
Fomu yenye maswali funge au wazi.
Umuhimu
Gharama ya chini.
Yaweza kutumika katika mahojiano.
Huokoa muda kwani mtafiti aweza kuituma na kuachia mhojiwa kujaza.
Hupatia habari za kuaminika na kutegemeka.
Udhaifu
Utata wa maswali kusababisha majibu yasiyo sahihi.
Si nzuri kwa wasiojua kusoma na kuandika.
Kutopata sifa za uwasilishaji kama vile kiimbo, toni na ishara.
Wahojiwa kukataa kuijaza kutokana na mwelekeo hasi dhidhi ya hojaji na hivyo kukwamiza utafiti.
Vifaa vya Kukusanya Fasihi Simulizi na Udhaifu Wake
Vinasa sauti/tepu rekoda
Kamera
Filamu na video
Diski za kompyuta
Kalamu na karatasi
Umuhimu
Kuweza kudumu na kufikia vizazi vingi.
Si rahisi kusahaulika-hubakia vile vile.
Si njia ghali kama vile video
Udhaifu
Sifa za uwasilishaji kama vile toni, kiimbo/toni na ishara haziwezi kuhifadhika hivyo kupotea.
Hupunguza hadhira kwa kulenga tu wanaojua kusoma na kuandika na hivyo kuathiri usambazaji wake.
Mbinu za Kuhifadhi Fasihi Simulizi
Huhifadhiwa na binadamu akilini k.m. ngano hupokewa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Katika maumbile au mazingira k.m. fisi daima huchechemea , kinyonga naye hutembea pole pole.
Katika vifaa meme k.m. nyimbo, hadithi, maigizo n.k. huweza kuhifadhiwa katika kanda za sauti, video, sidi na diski za kompyuta.
Katika michoro k.m. picha huhifadhi matukio maalum k.v. za kabila fulani likiwinda au likisherehekea.
Umuhimu wa Kukusanya/Kuhifadhi Fasihi Simulizi
Ili isipotee k.m. kwa kusahaulika.
Kuirekodi ili kuiendeleza kwa kuirithisha kwa vizazi vijavyo.
Ili kulinganisha fasihi simulizi za jamii mbalimbali na kuonyesha tofauti zake.
Ili kuhakikisha mtiririko katika uwasilishaji.
Kutunza historia ya jamii ili vizazi vijavyo viijue.
Ili kuziba mapengo ya utafiti yaliyomo kwa vile kuna tungo ambazo hazijatafitiwa kwa kina.
Kuendeleza elimu ya jadi ya jamii.
Kuingiliana na jamii iliyo chanzo cha fasihi humwezesha kuelewa na utamaduni na fasihi yake kwa ujumla
Humwezesha mwanafunzi kuona vipengele hai vya fasihi k.v. uigizaji, toni na kiimbo ambavyo husaidia kuielewa kwa kina.
Husaidia kuhifadhi tamaduni za jamii kwa nia ya kuzipitisha kwa vizazi vijavyo.
Husaidia kuelewa utamaduni wa jamii nyingine.
Humwezesha mwanafunzi kupata maarifa ya kufanya utafiti katika taaluma nyingine k.v. sosholojia.
Kujua fasihi simulizi za jamii nyingine humfanya mtafiti kuzielewa na kuzikubali jamii hizo na hivyo kuendeleza amani katika nchi.
Ili kusahihisha mawazo mapotovu kuhusu baadhi ya tanzu na vipera vya fasihi simulizi.
Matatizo Yanayomkabili Mkusanyaji wa Fasihi Simulizi
Gharama ya utafiti kuwa kubwa kiasi cha mtafiti kutoimudu k.v. kusafiria, kununulia vifaa.
Kutojaziwa hojaji kutokana na mtazamo hasi wa jamii dhidi ya ujazaji wake.
Wanajamii kukataa kutoa habari wakishuku mtafiti anawapeleleza au kwa kuona haya.
Wanajamii wengine kudai walipwe kabla ya kutoa habari na hivyo kukwamiza utafiti.
Mbinu nyingine k.v. hojaji huhitaji watu wanaojua kusoma na kuandika na ikiwa mhojiwa hajui utafiti utakwamizwa.
Uchache wa wazee na wataalamu wa fasihi simulizi kusababisha kukosekana au kupatikana kwa data isiyo ya kutegemewa.
Utawala kukataa kutoa idhini ya kufanya utafiti.
Kukosa ufadhili na utafiti kutofanywa kwa kutomudu gharama.
Muda wa utafiti kutotosha na hivyo kutopata habari za kutosha kuhusiana na mada yake.
Kikwazo cha mawasiliano ikiwa mtafiti na mhojiwa hawatumii lugha moja na mhojiwa hajui lugha nyingine na kumbidi mtafiti kukodi mkalimani na gharama kuongezeka.
Ukosefu wa vyombo vya usafiri kunakochelewesha utafiti na kutomalizika katika muda uliopangwa.
Ukosefu wa usalama k.v. kuvamiwa kwa kushukiwa anapeleleza na kuibiwa vifaa.
Changamoto Zinazokabili Ukusanyaji wa Fasihi Simulizi
Ukosefu wa utafiti wa kutosha kwani kuna vipera ambavyo bado havijaandikwa.
Uchache wa wataalamu wa kutafitia na kuendeleza utafiti.
Watu kuhamia mijini na kuingiliana na wa jamii nyingine na kufanya uhifadhi na urithishaji wa fasihi kutowezekana.
Mtaala wa elimu kupuuza lugha ya kiasili inayotumiwa kuhifadhia na kurithisha fasihi simulizi na hivyo kukatiza ukuaji wake.
Fasihi simulizi kuhusishwa na ukale na hivyo kutoona haja ya kuirithisha na kuihifadhi.
Kuhifadhiwa kwa fasihi simulizi akilini kusababisha kusahaulika, kubadilika hata kufa kwake.
Jinsi Jamii ya Sasa Inavyojaribu Kuhifadhi Fasihi Simulizi
Tamasha za muziziki kunakokaririwa na kuimbwa mashairi.
Sherehe za arusi, jando, mazishi mawaida.
Utegaji na uteguaji wa vitendawili kupitia redio na runinga.
Sarakasi za wasanii huhifadhi kipera cha vichekesho.
Ngoma za kienyeji kama isukuti katika hafla za kisiasa na harusi.
Utambaji wa hadithi hasa katika sehemu za mashambani.
Tanzu za Fasihi Simulizi
Tanzu ni aina za tungo zenye muundo uliokaribia kufanana.
hadithi
semi
ushairi
mazungumzo
maigizo
Kipera ni utungo wa fasihi simulizi unaowasilishwa mbele ya watu.
HADITHI
Masimulizi yanayotumia lugha ya mtiririko au nathari.
Sifa
Hutumia ya lugha ya mtiririko au nathari-kueleza matukio moja kwa moja.
Hurithishwa jamii kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Huwasilishwa mbele ya hadhira
Hutambwa mahali maalum k.v. ndani ya nyumba, chini ya mti, uwanjani, n.k.
Huweza kutokana na matukio halisi (kihistoria) au ya kubuni.
Huwa na mafunzo fulani kwa jamii/hadhira.
Hutumia wahusika wa aina tofauti k.v. nyumbani, wanyama, ndege, mazimwi, n.k.
Hutumia aina nyingine za sanaa k.v nyimbo, methali, ushairi, n.k.
Huwa na utendaji k.v. mtambaji kuiga fisi anavyokula.
Aghalabu hutambwa jioni.
Sababu za Ngano Kutambwa Jioni/Usiku
Ndio wakati watu walikuwa wamejumuika nyumbani baada ya kazi.
Utambaji ulikuwa njia ya kupitisha wakati chakula kikingojewa.
Wakati huu ulihakikisha mwanajamii hapotezi wakati wa kazi.
Majukumu ya Hadithi
Kufunza maadili yaliyo nguzo kuu kwa wanajamii.
Kukuza ujasiri wa kuzungumza hadharani.
Kuburudisha baada ya kazi ya kutwa.
Kukuza uwezo wa watoto wa kukumbuka ili kutamba baadaye.
Kueleza asili ya mambo k.m visaviini, visasili na ngano za usuli.
Kutahadharisha wanajamii dhidi ya kufanya mambo yasitofaa.
Kuunganisha watu katika jamii wanapojumuika pamoja kusikiliza utambaji.
Ngano za mtanziko hukuza uwezo wa kutathmini na kutoa uamuzi ufaao.
Kukuza lugha hasa kwa hadhira ya watoto.
Kuhifadhi na kuendeleza historia ya jamii k.v. mighani, tarihi, n.k.
Kuelimisha hadhira kuhusu utamaduni wao.
Njia ya kupokeza kizazi historia na utamaduni wa jamii.
Sifa za Mtambaji/Mganaji Bora
Asiwe mwoga ili kuweza kuzungumza hadharani.
Asiwe na haya ili kuweza kuzungumzia mambo ya aibu inapobidi.
Awe na uelewa wa mazingira na masuala ibuka katika jamii ili kuweza kuwasilisha dhana zisizopatikana katika mazingira yake k.m. kutumia rais kuelezea dhana ya mfalme.
Awe na ufahamu mpana wa lugha ili aweze kuitumia kwa uhodari na kuwasilisha kwa wepesi.
Awe mchanganfu na mcheshi ili kunasa makini ya hadhira na kuzuia isikinai.
Awe na ufahamu mpana wa utamaduni husika ili kuzuia kutumia maneno na ishara zinazoweza kuwaudhi au kupingana na imani za hadhira.
Awe na uwezo wa kushirikisha hadhira k.v. kuimba, maswali ya balagha ili isikinai, n.k.
Aweze kujua, matarajio, kiwango cha elimu na tajriba ya hadhira ili kuweza kubadilisha kwa kiwango kinachofaa.
Awe na uwezo wa kuingiliana vizuri na hadhira ili aivutie.
Awe na kumbukumbu nzuri ili usimulizi wake utiririke vizuri.
Awe na uwezo wa kudramatisha ili kuonyesha picha fulani k.v. kuiga toni, sauti, na kiimbo kulingana na swala analowasilisha.
Kubadilisha toni au kiimbo ili hadhira isikinai.
Awe na ujuzi wa kutumia ishara za uso, mwili na miondoko kulingana na hali anayoigiza.
Awe na ujuzi na ufasaha wa lugha ili kuwasilisha mawazo kwa njia mwafaka na inayovutia.
Aweze kubadilisha toni na kiimbo kulingana na hali tofauti anazoigiza k.v. huzuni
Awe na uwezo wa kushirikisha hadhira kwa nyimbo na maswali ya balagha ili kuondoa uchovu wa kutazama na kusikiliza.
Awe na uwezo wa ufaraguzi/ kubadilisha utambaji wake papo hapo kutegemea hadhira yake na kutoa mifano inayofahamika kutoka katika mazingira ya hadhira.
Awe na uwezo wa kutumia mtuo wa kidrama ili kuongeza taharuki, kusisitiza ujumbe na kuteka makini ya hadhira.
Aina za Hadithi
Hadithi za Kubuni
Hazisimulii matukio ya kweli bali ya kutungwa
Hadithi za Kisalua/Kihistoria
Zinazosimulia matukio yaliyowahi kutendwa na wahusika waliowahi kuishi.
Huongezewa ubunifu ili kuvutia zaidi.
Hadithi za Kubuni
Ngano
Hadithi zinazosimulia kisa chenye funzo na zenye wahusika aina ya binadamu, viumbe na vitu visivyo na uhai.
Sifa za Ngano
Zina fomyula ya kuanzia/mwanzo maalum.
Zina fomyula ya kumalizia/mwisho maalum.
Zina wahusika aina mbalimbali.
Zina matumizi ya nyimbo.
Hutumia takriri (usambamba) ili kusisitiza k.m. zimwi likakimbia, likakimbia.
Huwa na na maadili/mafunzo
Hutumia maswali ya balagha kuongeza taharuki.
Hutumia tanakali za sauti.
Zina matumizi ya fantasia au matukio yanayokiuka uhalisi/mambo ya ajabu k.v. binadamu kuruka kama ndege, zimwi kumeza watu na baadaye kutapika wote, n.k.
Kutambua mbinu zilizotumiwa katika hadithi/ngano
Kutambua wahusika
Aina za Fomyula za Kuanzia/Mianzo Maalum
Paukwa, Pakawa. Sahani. Ya mchele. Giza. La mwizi. Na kiboko je? Cha mtoto mrorofi…
Hapo zamani za kale/za kongamawe…
Ilitokea…
Hadithi! Hadithi! Hadithi njoo…
Kaondokea chenjangaa, kajenga nyumba kakaa, mwanangu mwanasiti, kijino kama chikichi, cha kujengea kikuta, na vilango vya kupita…
Hapo jadi na jadudi…
Umuhimu wa Fomyula ya Kuanzia/Mwanzo maalum
Kuvuta makini ya hadhira.
Kumtambulisha mtambaji kwa hadhira.
Kuashiria mwanzo wa hadithi.
Kutoa hadhira kutoka ulimwengu halisi hadi ule wa hadithi.
Aina za Fomyula za Kumalizia/Miishio Maalum
Hadithi inaishia hapo.
Tangu siku hiyo…
Wakaishi raha mustarehe.
Maadili
Umuhimu wa Fomyula ya Kumalizia/Mwisho Maalum
Kuashiria mwisho wa hadithi.
Kutoa hadhira katika ulimwengu wa hadithi hadi ule halisi.
Kumpisha/kumpa fursa mtambaji anayefuata.
Kupisha shughuli inayofuata.
Kutoa funzo la hadithi kwa muhtasari.
Kupa hadhira nafasi ya kupumzika baada ya kuwa makini kwa muda.
Umuhimu wa Nyimbo katika Ngano
Kushirikisha hadhira.
Kusisimua hadhira na kuondoa ukinaifu
Kuteka makini yao.
Kuwasilisha mafunzo/maadili.
Kutenganisha matukio katika hadithi.
Kuburudisha hadhira.
Kupunguzia hadhira mwemeo.
Umuhimu wa Tanakali za Sauti/Onomatopeya katika Ngano
Kuongeza utamu.
Kusaidia msomaji kupata picha kamili.
Kusaidia kupata hisia halisi
Aina za Ngano
Hurafa
Hadithi zenye wahusika wanyama na ndege.
Hurafa za kijanja ni hadithi ambapo wanyama wadogo hutumia ujanja wa hali ya juu ili kujinasua na hali ngumu au mitego wanayotegewa.
Sifa
Wahusika ni wanyama au na au ndege.
Wanyama na ndege hupewa sifa za binadamu
Ni kazi ya ubunifu.
Hutoa mafunzo kwa njia ya kuchekesha na isiyoumiza.
Huwa na ucheshi mwingi.
Hutumia mbinu ya uhuishi.
Huwa na sifa zinazohimizwa na zinazoshutumiwa.
Ujanja au uongo hujitokeza katika hurafa za kijanja.
Ushindi hujitokeza katika hurafa za kijanja.
Umuhimu
Kutahadharisha watu dhidi ya kuwa wa danganyifu/kudanganyika kwa urahisi.
Kuonyesha jinsi tabia ya udanganyifu inavyoweza kujitokeza na kuathiri watu.
Hurafa za kijanja hufunza jinsi ya kupampana na hali ngumu.
Hekaya/Ngano za Kiayari
Hadithi zinazomsawiri mhusika anayetumia ulaghai kupata matilaba yake kutoka kwa wengine (Abunuwasi).
Sifa
Wahusika wakuu ni binadamu.
Huwa na ubunifu mkubwa.
Hustaajabisha na kuchekesha.
Ujanja na uongo hujitokeza.
Ushindi hujitokeza.
Ni za kubuni.
Umuhimu
Hutahadharisha watu dhidi ya kuhadaika kwa wepesi.
Huonya dhidi ya matokeo yanayoweza kuwapata wanaojinyakulia mali kwa udanganyifu.
Kuonya dhidi ya usaliti.
Kukashifu viongozi dhalimu na matendo maovu.
Kukejeli wanaotumia nguvu badala ya akili/hekima.
Visasili
Hadithi zinazoeleza asili ya matukio fulani katika jamii k.m. kifo, jua, lugha, zilizala n.k.
Sifa
Husimulia mambo ya kiimani na kidini.
Huwa na misingi ya kihistoria.
Hueleza asili ya matukio katika jamii.
Wahusika ni wanyama na binadamu.
Huwa na maadili.
Hurithishwa kizazi hadi kingine.
Umuhimu
Kueleza asili ya mambo kama vile kifo, utamaduni n.k.
Kueleza utaratibu wa kutekeleza desturi k.v. mahari.
Kuhalalisha baadhi ya mila na desturi za jamii k.v. ulipaji mahari, uabudu miti, n.k.
Kukitisha mizizi imani fulani ya watu.
Kupunguza athari za majanga kama vile kuhalalisha kifo.
Kutambulisha jamii kwani kila jamii ina aina yake ya visasili.
Kuhifadhi historia na utamaduni wa jamii
Ngano za usuli
Hadithi zinazoeleza asili ya hali, tabia, mahusiano au wasifu. k.v. asili ya kuku kuchakura, asili ya kinyonga kwenda kwa tahadhari, n.k.
Sifa
Wahusika ni wanyama na binadamu
Ni kazi ya kubuni.
Hueleza kuhusu asili ya sifa, tabia au hali.
Hutumia mbinu ya uhuishi.
Huwa na maadili.
Umuhimu
Kueleza sababu ya tabia, hali au sifa Fulani.
Kuonya dhidi ya tabia hasi kama vile ulafi.
Ngano za mazimwi
Hadithi ambazo wahusika ni mazimwi.
Sifa
Wahusika ni mazimwi
Mazimwi huwakilisha sifa hasi za binadamu k.m ulafi, ukatili, uovu n.k.
Hujaa uharibifu.
Huwa na matumizi mengi ya fantasia.
Kipengele cha safari hujitokeza k.v. kwenda nchi za mbali kutafuta suluhisho.
Ushindi hujitokeza (mazimwi hushindwa).
Ni kazi ya kubuni.
Huwa na maadili.
Mazimwi huwa na sifa zinazokiuka mipaka ya binadamu k.m. kinywa kisogoni, jicho moja kubwa, n.k.
Umuhimu
Kukashifu tabia ya uovu, ulafi, na ukatili.
Kutahadharisha dhidi ya kuwa na ulafi, ukatili n.k.
Kutia moyo waliodhulumiwa kuwa waliowanyanyasa wataadhibiwa siku moja.
Ngano za Mashujaa
Ambazo zinazohusu watu waliotenda matendo ya kishujaa katika jamii zao kama vile kuokoa jamii.
Sifa
Kipengele cha motifu au kusafiri nchi za mbali, kupigana na mazimwi kuokoa jamii.
Husawiri mapigano kati ya wema (lila) na ubaya (fira).
Uovu huwakilishwa na mazimwi au viongozi dhalimu
Hatimaye wema hushinda uovu kwa juhudi za mashujaa
Ngano za mashujaa ni za kubuni ilhali katika mighani, mashujaa wanaaminiwa waliishi.
Umuhimu
Kuhimiza uzalendo na ujasiri miongoni mwa vijana.
Kuhimiza ujasiri miongoni mwa vijana.
Kusifu mashujaa katika jamii
Kuelimisha jamii kwa kuwapa maarifa ya kukabiliana na changamoto, inda na ila.
Kuhimiza uzalendo kwa kuhimiza watu kuiga mashujaa na kupigania jamii.
Kuonya dhidi ya matendo hasi k.v. ukatili.
Kuhimiza watu kutokata tamaa
Ngano za mtanziko
Hadithi ambapo mhusika hukabiliwa hali ngumu ya kuamua baina ya mambo wawili au zaidi yanayomkabili.
Sifa
Wahusika ni wanyama au binadamu.
Ni kazi ya kubuni.
Mhusika hulazimika kufanya uteuzi mgumu.
Hali mbili au zaidi zinazotatanisha huwepo.
Umuhimu
Hutuerevusha jinsi ya kupambana na hali ngumu.
Kuonya/kutahadharisha dhidi ya kujiponza.
Kukuza uwezo wa kupima mambo na kuteua lililo muhimu.
Kuonya dhidi ya kutenda bila kuwaza kwa kina.
viii) Ngano za Kimafumbo
Ambazo huwa na maana ya ndani/iliyofichika.
Istiara
Hadithi ambayo maana yake huwakilisha maana nyingine iliyofichika k.v. hurafa ambapo wanyama huwakilisha binadamu.
Mbazi
Hadithi fupi inayotolewa inayotolewa kama mfano kumkanya au kumwelekeza mtu k.v. katika biblia.
Hadithi za Kisalua/Kihistoria
Mighani
Hadithi za mashujaa/majagina wa jamii fulani k.m. Rwanda Magere wa Waluo, Fumo Liyongo wa Wapate, Koome Njue wa Wameru, Wangu wa Makeri wa Wakikuyu na Syokimau wa Wsakamba.
Sifa
Huhusu mashujaa wa jamii fulani.
Wahusika hupambana na hali ngumu inayosababishwa na maadui.
Wahusika hupewa sifa na uwezo usiokuwa wa kawaida k.v. ukubwa wa ajabu, nguvu katika kivuli, nguvu katika nywele, kutoulika n.k.
Wahusika hupigania haki za wanyonge.
Mhusika hukomboa jamii yake dhidi ya maadui.
Mhusika hufa kifo cha huzuni (tanzia) kwa kusalitiwa na mtu wa karibu k.v. mwanamke au jamaa zao.
Mashujaa huuliwa kwa njia ya ajabu kama vile kunyolewa nywele, kivuli kuchomwa mkuki, kuchomwa shindano ya shaba kitovuni
Mighani huzungumzia matukio ya kihistoria.
Kuna tabia ya kupiga chuku matukio yaliyo hadithini.
Mighani hurithishwa jamii kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Huchukuliwa na jamii kama hadithi zenye ukweli na jamii hujinasibisha na mighani hiyo.
Husimulia mambo ya kiimani na kidini.
Umuhimu
Kutambulisha jamii kwani kila jamii ina aina yake ya mighani.
Kuhifadhi na kumbusha historia yajamii.
Kusifu mashujaa katika jamii.
Kuhimiza ujasiri miongoni mwa vijana.
Kuelimisha jamii kwa kuwapa maarifa ya kukabiliana na adui au changamoto.
Kukuza uzalendo kwa kuhimiza watu kuiga mashujaa na kupigania jamii.
Kuonya dhidi ya matendo hasi kama vile usaliti.
Kuhimiza watu kutokata tama.
Tofauti Kati ya Mighani na Visasili
mighani
visasili
Þ Husimulia kuhusu mashujaa.
Þ Husimulia historia ya jamii.
Þ Wahusika wakuu ni majagina.
Þ Hueleza sifa za majagina.
Þ Husimulia asili ya vitu.
Þ Husimulia mianzo ya vitu au mambo.
Þ Wahusika ni k.v. binadamu, miungu, wanyama, n.k.
Þ Hueleza mianzo ya desturi.
Visakale
Masimulizi ya matukio yaliyotendeka zamani k.v. vita, majanga kama njaa na magonjwa na hamahama za jamii k.v. waisraeli kutoka misri.
Visaviini
Hadithi zinazoeleza chimbuko la jamii Fulani
Mapisi
Maelezo ya kihistoria yasiyo na ubunifu wowote k.v. chimbuko la kundi la wabantu kutoka Afrika ya Kati na kuenea sehemu mbalimbali za Afrika.
Tarihi
Maelezo kuhusu matukio ya kihistoria kulingana na yalivyofuatana ki wakati
Kumbukumbu
Maelezo ya kitawasifu kuhusu mtu au jamii inayotambulika kwa kutoa mchango fulani mkubwa.
Vipera Vingine vya Hadithi
Soga
Hadithi fupi za kuchekesha zinazolenga kutania au kudhihaki.
Sifa
Wahusika ni wa kubuni.
Hutaja ukweli unaoumiza.
Hutumia vichekesho kupunguza ukali wa dhihaka.
Hutumia chuku kupita kiasi.
Huhusu tukio moja.
Ni fupi.
Umuhimu
Kukashifu matendo hasi kwa njia ya ucheshi
Kuonya na kutahadharisha dhidi ya matendo hasi k.v. ulaghai.
Kufunza maadili.
Kuburudisha kwa kuchekesha.
Vigano
Hadithi fupi zinazosimulia kuhusu matendo mabaya katika jamii na wakati uo huo kuonya na kuelekeza dhidi yayo.
Aghalabu huandamana na methali kwa lengo la kufafanua linalokusudiwa au kudhibitisha funzo la methali fulani.
Sifa
Huwa vifupi.
Husimulia kisa kimoja tu.
Wahusika ni binadamu na wanyama.
Hufunza maadili kutokana na methali.
Kisa
Masimulizi mafupi yenye tukio moja lenye funzo kwa njia ya kufurahisha.
Mambo ya Kuzingatia katika Uchambuzi wa Hadithi/Ngano
Kueleza aina ya ngano kwa kuzingatia wahusika na maudhui
Ngano yaweza kuwa ya mazimwi na ya mashujaa kwa wakati mmoja.
Ngano yaweza kuwa hurafa, ya usuli na ya kiayari.
Kutaja wahusika
Kufafanua sifa za wahusika wakuu
Maadili/mafunzo yanayojitokeza katika hadithi
Kubainisha sifa za ngano/hurafa/hekaya, n.k. zinazojitokeza katika hadithi.
Kueleza umuhimu wa fomyula ya kuanzia/wimbo uliotumiwa katika hadithi.
Kubainisha tamathali za usemi zilizotumiwa katika hadithi fulani
Kuonyesha jinsi ngano inavyoshughulikia maudhui fulani.
Kufafanua ufaafu wa methali fulani zilizotumiwa katika hadithi.
Katika ngano ya mtanziko, ungekuwa mhusika mkuu ungefanya nini?
Mbinu za Lugha/Fani /Tamathali za Usemi katika Fasihi
Maneno au vifungu vya maneno vinavyotumiwa kutia fasihi urembo ili kufanya ujumbe ueleweke vyema zaidi.
Aina
Tashbihi
Ulinganishi kwa kutumia viunganishi kama, mithili, mfano na sawa.
Sitiari/ Istiara
Ulinganishi usio wa moja kwa moja.
Tashhisi/Uhaishaji
Kukipa kitu sifa ya uhai.
Taashira/ Ishara
Kitu kuwakilisha kingine.
Chuku/udamisi
Kutia chumvi au kufanya kitu kionekane kikubwa sana au kidogo sana.
Takriri
Urudiaji wa neno au mafungu ya maneno.
Tanakuzi
Maneno yaliyo kinyume
Tabaini
Msisitizo kwa njia ya kinyume kwa kutumia kikanushio si.
Ritifaa
Kusemesha asiyekuwapo kama yupo.
Taharuki
Kuacha msomaji akiwa na hamu ya kutaka kujua kipi kitakachojiri halafu.
Majazi
Majina yanayooana na sifa za wahusika, vitu au mahali.
Mbinu rejeshi
Kukumbusha mambo yaliyopita.
Methali
Semi fupi ambazo hueleza kwa muhtasari au mafumbo ukweli fulani wa kimaisha.
Nahau
Fungu la maneno lenye maana tofauti na maana ya kawaida ya maneno hayo.
Misemo
Semi zinazobeba ukweli wa kujumla Mifano:
Mdokezo
Mambo kuachwa bila kumalizwa.
Balagha
Maswali yasiyohitaji majibu.
Taswira
Ujenzi wa picha akilini.
Kinaya
Mhusika kutumia maneno au matendo yaliyo kinyume cha inavyotarajiwa.
Koja
Kuorodhesha maneno na vitenzi kwa kutumia koma.
Kejeli
Kudharau au kubeza.
Jazanda
Kufananisha vitu kwa mafumbo k.m. katika biblia.
Nidaha/ Siyahi
Maneno ya kuonyesha hisia za moyoni.
Tanakali/onomatopeya
Miigo ya sauti zinazotokea baada ya kitendo.
Uzungumzi nafsia
Kujisemesha mwenyewe.
Dayalojia
Utohozi/ Uswahilishaji
Kuchanganya ndimi
Kutumia lugha ngeni.
Tafsida/usafidi
Kutumia lugha ya adabu au kupunguza ukali wa maneno.
Mkengeuko
Kwenda kinyume na matakwa ya jamii k.v. usenge, ndoa ya watu wasio wa rika rika moja, mapenzi nje ya ndoa.
ulinganuzi
Kuweka pamoja mambo yanayopingana ili kulinganisha
Kweli kinzani
Hoja mbili zinazopingana/kutowezekana.
Matumizi ya Lugha Katika Methali
Sitiari
Mgeni ni kuku mweupe.
Ahadi ni deni.
Upweke ni uvundo.
Mgeni ni kuku mweupe.
Ujana ni moshi.
Mapenzi ni kikohozi.
Kukopa arusi kulipa matanga.
Tashbihi
Kawaida ni kama sheria.
Riziki kama ajali ijapo huitambui.
Usilolijua ni kama usiku wa giza.
Ufalme kama mvua hupiga na kupita.
Tashhisi
Siri ya mtungi muulize kata.
Paka akiondoka panya hutawala.
Jembe halimtupi mkulima.
Ukupigao ndio ukufunzao.
Adhabu ya kaburi aijuaye maiti.
Takriri
Haba na haba hujaza kibaba.
Chovya chovya humaliza buyu la asali.
Hauchi hauchi unakucha.
Hayawi hayawi huwa.
Mtoto wa nyoka ni nyoka.
Bandu bandu huisha gogo.
Balagha
Pilipili usiyoila yakuwashiani?
Angurumapo samba mcheza ni nani?
Wameshindwa wenye pembe seuze wewe kipara?
Simba mla watu akiliwa huwani?
Mzigo uko kichwani, kwapa lakutokeani jasho?
Mavi usiyoyala wayawingiani kuku?
Mla ni mla leo mla jana kalani?
Taswira
Mpanda farasi wawili hupasuka msamba.
Mti mkuu ukigwa wana wa ndege huyumba.
Mtupa jongoo hutupa na ung`ong`o wake.
Angeenda juu kipungu hafikii mbingu.
Chuku
Mzigo wa mwenzio ni kanda la sufi.
Maji ya kifuu bahari ya chungu.
Usipoziba ufa utajenga ukuta.
Tanakali za sauti
Chururu si ndondondo!
Ndo! Ndo! Hujaza ndoo.
Kiliacho pa kijutie.
Kinaya
Bara Hindi ndiko kwenye nguo na waendao uchi wapo.
Kwenye miti hakuna wajenzi.
Asante ya punda ni mateke.
Kigumba kwa nguruwe kwa binadamu ki uchungu.
Kikiharibika cha fundi kikiongoka cha bwana Sudi.
Kejeli/dhihaka/stihizai
Umekuwa mung`unye waharibikia ukubwani.
Hawi Musa kwa kubeba fimbo.
Ucha Mungu si kilemba cheupe.
Kichwa cha kuku hakistahili kilemba.
Kichwa cha nyoka hakibandikwi mtungi.
Jazanda
Joka la mdimu hulinda watundao
Mtu mwovu huwanyima wengine vitu asivyovihitaji.
Kupanda mchongoma kushuka ndio ngoma
Ni rahisi kujitia katika matata kuliko kujitoa.
Taashira
Kimya kingi kina mshindo mkubwa.
Kuku mgeni hakosi kamba mguuni.
Kweli kinzani
Wagombanao ndio wapatanao.
Ukupigao ndio ukufunzao.
Kuinamako ndiko kuinukako.
Mwenye kelele hana neno.
Kimya kingi kina mshindo mkubwa.
Tanakuzi
Tamaa mbele mauti nyuma.
Mpanda ngazi hushuka.
Usione kwenda mbele kurudi nyuma si kazi.
Kuainisha methali kutokana na matumizi ya lugha ni kusema mbinu ambazo imetumia.
Vigezo vya Kuainishia Methali/Kuziweka Pamoja na kuzichambua
Mandhari/mazingira k.m. kilimo.
Ukipanda pantosha utavuna pankwisha.
Jembe halimtupi mkulima.
Maudhui k.m. ulezi
Samaki mkunje angali mbichi.
Mcha mwana kulia hulia yeye
c) fani/tamathali k.m. takriri
Haba na haba hujaza kibaba
Mtoto wa nyoka ni nyoka.
d) Jukumu k.m. kuonye
Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
Ukiambiwa jiambie usijeishia kumbe.
Maana k.m. sawa
Haraka haraka haina baraka.
Polepole ndio mwendo.
Vigezo zaidi vya kuchambua methali
Inarejelea vitu gani? K.m. Hindi ndiko kwenye nguo na waendao uchi wapo.
Nchi-Hindi
Vitu-nguo
Watu-waendao uchi
Inakupa wazo gani kuhusu jamii husika?
Utamaduni na njia za kiuchumi.
Vitendawili
Semi ambazo hutolewa kwa mtu kwa mfano wa swali ili azifumbue.
Sifa
Huwa vifupi kimaelezo.
Hutumia lugha ya kimafumbo.
Hutolewa mbele ya hadhira.
Hutumia ufananisho wa kijazanda.
Kunazo huhusiana na methali k.m. mzee amekufa vyombo vimevunjikavunjika.
Huwa na wakati maalum wa kutolewa yaani jioni.
Huwa na mchezo wa maneno k.m. Ukiona njigi utadhani njege.
Maziwa na tui
Hujisimamia vyenyewe.
Kunavyo huwa na jibu zaidi ya moja k.v. Gari la kila mtu
miguu, kifo au jeneza
Hutumia tamathali za lugha kwa ufanifu mkubwa
Huweza kuwa na fomyula/muundo maalum
Mteguaji: Kitendawili
Mteguaji: Tega
Mteguaji: Kitendawili chenyewe- Popoo mbili zavuka mto
Mteguaji : Mlango
Mtegaji: Umenoa. Nipe mji.
Mteguaji: Ninakupa Nairobi.
Mteguaji: Nilienda Nairobi watu wa Nairobi wakaniambia nije niwasalimu. Jibu ni macho.
Umuhimu
Kuburudisha jioni baada ya kazi.
Kukuza ubunifu wa kuvitunga kwa kulinganisha vitu katika mazingira ili kuviunda.
Kuimarisha uwezo wa kukumbuka.
Kukuza uwezo wa kufikiri kwani mfumbiwa huhitaji kufikiri sana ili kupata jibu.
Kuleta umoja na ushirikiano katika jamii kwa kuleta watu pamoja wakati vinategwa.
Kuimarisha ujuzi wa kujieleza kwa lugha.
Kupanua ujuzi wa mazingira wa mtoto.
Kuendeleza utamaduni wa jamii k.m. Nyumbani mwetu mna papai lililoiva lakini. siwezi kulichuma
Ndugu wa kiume asimuoe nduguye wa kike.
Kukejeli au kudharau tabia mbaya k.m. Wazungu wawili wanachungulia dirishani
makamasi
Aina za vitendawili
Sahili
Vina muundo rahisi/maneno machache k.m Akiona mwangaza wa jua hufa-samaki.
Tata
Vyenye majibu tofauti
Kisimulizi
Masimulizi k.m. Kulikuwa na baba ng’ambo moja ya mto na binti zake wawili ng’ambo ya pili. Alikuwa na maembe mawili aliyopaswa kuyavukisha pamoja apelekee binti zake. Angefanya nini?
Vya tanakali k.m. Parrrr! Mpaka Makka-utelezi.
Mkufu
Vyenye sehemu zinazochangizana kimaana k.m. Nikitembea yuko lakini nikiingia nyumbani hupotea-kivuli.
Matumizi ya Lugha Katika Vitendawili
Tashhisi
Amefunika kote kwa blanketi lake jeusi-giza.
Akivaa nguo hapendezi, akiwa uchi hupendeza mno-ndizi.
Anakula lakini hashibi-kifo/mauti.
Amchukuapo hamrudishi-kaburi.
Akizungumza kila mtu hubabaika-radi.
Daima nasababisha mafarakano-uke wenza.
Tashbihi
Boi wangu kazama kaibuka kama mzungu-mwiko wa ugali.
Sitiari
Bibi hatui mzigo-konokono.
Mamangu hachoki kunibeba-kitanda.
Fatuma mchafu-ufagio.
Saa yetu kadiri inavyotembea ndivyo inavyopunguza nguvu-moyo.
Mzungu kujishika kiuno- kikombe.
Nina mapapai yangu mawili ambayo siwezi kuyala- matiti ya mwanamke.
Ng`ombe wangu nisipomshika mkia hali nyasi-jembe.
Kitu changu kitumiwacho na wengine kuliko mimi-jina.
Popoo mbili zavuka mto-macho.
Gari la kila mtu-miguu.
Dada ni mrembo lakini akiguzwa analia-papai.
Takriri
Huku ng`o na kule ng`o-giza.
Amezaliwa Ali, amekufa Ali, amerudi Ali-nywele.
Huku fungu katikati bahari-naz.i
Tanakali
Parrr! Mpaka Makka-utelezi.
Huku pi kule pi-mkia wa kondoo atembeapo.
Ba funika ba funua (Bak bandika, bak bandua)-nyayo.
Tang! Yaanguka-sarafu.
Kweli kinzani
Ana meno lakini hayaumi-kitana.
Ajenga ingawa hana mikono-ndege.
Hukopa lakini halipi-kifo.
Nina shamba langu kubwa lakini nikivuna halijai hata kofi-nywele.
Hufa akifufuka-bahari kupwa.
Nameza lakini sishibi-mate.
Taswira
Adui tumemzingira lakini hatumwezi-moto.
Nyama nje, ngozi ndani, mchanga ndani-firgisi ya kuku.
Wanatazamana tu lakini hawaamkiani-ardhi na bingu.
Askari wangu wote wamevaa kofia upande-mahindi shambani.
Samaki wangu aelea kimgongomgongo-merikebu.
Babu amebeba machicha meupe kichwani- mvi.
Stihizai/dhihaka/kejeli
Akivaa miwani hafanyi kazi vizuri-mlevi.
Mzungu anachungulia dirishani-makamasi.
Uzi mwembamba umefunga dume-usingizi.
Mtani wangu hata akiishi majini hatakati-chura.
Kisiki chetu hakikui-mbilikimo.
Nimemuona bi kizee amejitwika machicha-mvi.
Jazanda
Mungu alinipa shilingi mbili, moja nitumie nyingine niweke-ardhi na mbingu.
Kuchambua kitendawili kwa kueleza mbinu za lugha zilizokiunda.
Kulinganisha vitendawili na methali
Kufanana
Zote mbili ni tungo fupi.
Zote mbili huwa na maana fiche.
Zote mbili hutumia lugha inayojenga taswira.
Zote mbili hupata maana kulingana na jamii.
Zote mbili Huwa na muundo maalum.
Zote mbili hufumbata ukweli fulani wa kijamii.
Tofauti
Vitendawili
Methali
ü Vina fomyula maalum ya uwasilishaji.
ü Fumbo lazima lifumbuliwe papo hapo.
ü Maarufu zaidi miongoni mwa watoto/vijana.
ü Hutolewa katika vikao maalum.
ü Hadhira tendi inayotoa maana
ü Hutumia lugha ya majibizano.
ü Hazina fomyula.
ü Fumbo halifumbuliwi papo hapo.
ü Kuonyesha hekima hasa miongoni mwa watu wazima na wazee.
ü Si lazima zitengewe vikao.
ü Hadhira si tendi.
ü Kauli moja ya msemaji
Chemsha Bongo
Maswali ambayo huhitaji mtu kutumia akili na ujuzi kuyajibu.
Mafumbo ni kauli zenye maana iliyofichika na hujumuisha vitendawili na chemshabongo.
Mifano
Kilo moja ya chuma na kilo moja ya nyama ipi nzito?
Amada ana wafanyikazi saba, wanne hufanya kazi vizuri, wawili ni kama wamekufa, mmoja ni kama mwenda wazimu- miguu, pembe na mkia wa ng’ombe.
Kipungu alipita juu, mama na ndege wawili wakamwangalia. Je macho mangapi yalimuona kipungu?- manne.
Nina watu wangu watatu, wawili ni watoto na wawili ni baba- mtoto, baba na babu.
Chura alitumbukia katika shimo la futi 30 na anaruka futi 10. Aruke mara ngapi ili atoke?- Hawezi.
Watu watatu wanavuka mto. Mmoja aliyaona maji na kuyakanyaga. Wapili aliyaona lakini hakuyakanyaga. Watatu hakuyaona wala kuyakanyaga. Watu hao ni kina nani?
Sifa
Ni kauli fupi au ndefu.
Hutuia lugha ya kimafumbo.
Hutumia ufananisho wa kijazanda.
Huhitaji mtu kuwaza ili kupata jibu.
Hujengwa na vitu vinavyotokana na mazingira.
Hazina muundo maalum kama methali, nahau na vitendawili
Hupima uwezo wa msikilizaji wa kutambua jambo lililofichwa.
Umuhimu
Kuimarisha stadi ya kusikiliza.
Kunoa uwezo wa kufahamu.
Kutoa mawaidha.
Kufunza kuhusu maumbile.
Kuimarisha uwezo wa kukumbuka.
Kufunza mambo kuhusu mazingira na maumbile.
Kukuza uwezo wa kutumia lugha.
Kukuza uwezo wa kufikiri.
Kuburudisha na kuchekesha.
Kukuza uwezo wa kubuni.
Vitanza Ndimi
Sentensi zenye mfuatano wa sauti zinazotatanisha kimatamshi zinapotamkwa kwa haraka.
Mifano
Wataita wataita Wataita wa Taita.
Waite wale wana wa liwali wale wali wa liwalii
Kupa mpe akupao kumpa asokupa si kupa ni kutupa.
Shirika la Reli la Rwanda limefungwa.
Hilo lililoliwa ndilo nililolitaka.
Mchuuzi wa mchuzi hana ujuzi wa mjusi wa juzi.
Cha mkufuu mwanafuu ha akila hu cha mwanafuu mkufuu hu akila ha
Pema usijapo pema ukipema si pema tena
Nguo zisizotakikana zitachomwa zote.
Sifa
Ni kauli fupi.
Huwa na mchezo wa maneno.
Huundwa kwa sauti zinazokaribiana kimatamshi.
Hutumia maneno yenye maana zaidi ya moja au yenye sauti sawa.
Hutanza/hutatiza ndimi za wengi wakalemewa kutamka.
Hukanganya kimatamshi.
Umuhimu
Kukuza matamshi bora mtu anapoendelea kutamka.
Kukuza uwezo wa kufikiri haraka ili kujua maana za maneno ili kutamka ipasavyo.
Kupanua ujuzi wa msamiati.
Kuburudisha kwa kufurahisha na kuchangamsha.
Husaidia kutofautisha maana za maneno.
Kujenga stadi ya kusikiliza.
Kukuza ubunifu kwa kuteua maneno yanayotatanisha kisauti na kimaana.
Kujenga uhusiano bora kwa ucheshi.
Lakabu
Jina la msimbo/kupanga/ambalo mtu hupewa au hujipa kutokana na sifa zake.
Asili ya Lakabu
Tabia
Sifa za kimaumbile
Matendo
Nasaba atokayo mtu.
Tabaka
Jinsi mtu anavyotamka maneno k.m. ung’eng’e.
Mifano
Nyayo
Moi
Simba wa Yuda
Haille Selassie
Mkuki uwakao
Kenyatta
Nyundo/Tingatinga
Raila
Baba wa taifa
Rais
Mama wa Taifa
Mke wa Rais
Sifa
Huwa neno au fungu la maneno kadha.
Huwa na maana iliyofumbwa.
Huoana na sifa hasi au chanya za aliyepewa.
Huwa za kusifu au kudhihaki.
Huweza kudumu hata kusahaulisha jina halisi la mtu.
Hutumia sitiari k.m. chui kumaanisha mkali.
Hutumia taswira.
Hushika sana kimatumizi miongoni mwa watu.
Umuhimu
Kufahamisha sifa za mtu kwa kifupi.
Huwa njia ya washairi ya kujitangaza bila kujisifu moja kwa moja.
Hutumiwa kama ishara ya heshima kwa anayestahili heshima k.m. kiongozi.
Kuficha utambulisho au jina halisi la mtu.
Hutumiwa katika majigambo na mhusika kuonyesha ubingwa wake.
Kuficha siri ili anayemrejelewa asijulikane k.m. kikulacho.
Kukuza uhusiano bora miongoni mwa watani wanaporejeleana kwa lakabu.
Kusifu tabia njema kwa kumpa mtu lakabu nzuri.
Kudhihaki au kukashifu tabia mbaya kwa kumpa mtu lakabu mbaya
Kutambulisha asili ya mtu.
Misemo
Semi zinazobeba ukweli wa kijumla.
Mifano
Binadamu ni udongo.
Mwili haujengwi kwa mbao.
Umaskini si kilema.
Lila na fira havitangamani.
Ndio kwanza mkoko ualike maua.
Mambo kuzidi kushika kasi.
Mgomba haupandwi changaraweni ukamea
Jambo halifanywi mahali pasipofaa likapendeza.
Sifa
Hutumia lugha ya muhtasari.
Hutoa ukweli kwa jumla.
Hazina muundo maalum.
Umuhimu
Kusisitiza ujumbe.
Kuongeza utamu katika lugha.
Kusisitiza jambo fulani.
Kufunza maadili au kuhimiza.
Kuchochea hisi fulani.
Nahau
Fungu la maneno lenye maana tofauti na maana ya kawaida ya maneno hayo.
Mifano
Kuasi ukapera
kuoa
Kupiga vijembe
sema kwa mafumbo
Ndege mbaya
bahati mbaya
Kidudu mtu
mfitini
Paka mafuta kwa mgongo wa chupa
Danganya au hadaa mtu
Visha kilemba cha ukoka
Mpa mtu sifa za uongo ili umpumbaze
Kubali shingo upande
Kuyavulia maji ngu
kumaliza jambo fulani ulilolianzia
Arusi ya ndovu kumla mwanawe
kubwa
Sifa
Hutumia lugha ya kimkato.
Maneno huwa na maana tofauti na ya kawaida.
Kunazo huwa na maana zaidi ya moja k.v. kuja jamvi-kumaliza shughuli au kuondoka.
Huundwa kwa neno moja, mawili au zaidi.
Huibua taswira.
Zina muundo maalum/huundwa kwa aina mbalimbali za maneno.
T+T
kufa kupona
kufumba na kufumbua
T+N
kupiga domo
kata kamba
T+E
Kujikaza kisabuni
kufa kiofisa
N+N
donda dugu
domo kaya
N+V
nyota njema
dege mbaya
N+T
damu kumkauka
akili kumruka
Umuhimu
Kukuza na kuendeleza msamiati wa maneno.
Kupunguza ukali wa maneno (tafsida).
Kuongeza utamu/ladha katika lugha.
Kuhifadhi siri kwani sio wote wanajua maana.
Kujaribu uwezo wa msikilizaji kufichua maana iliyofichika.
Misimu/simo
Semi ambazo huzuka katika mazingira na kipindi fulani.
Aina za Mizimu
Inayotumika na kutoweka
Inayokita kimatumizi kuingizwa katika Kiswahili sanifu k.m. toa chai, chokora, n.k.
Asili
Ufupishaji maneno
komp
Utohozi
Fathee
hepi
Sitiari/jazanda
nyani-mlinda lango
fisi- mlafi
Tanakali
mtutu- bunduki
ndala- malapulapu
Uundaji maneno mapya
hanya
Kupa maneno maana mpya
chuma-gari
toboa- faulu
Kugeuza maneno
risto-stori
Kuboronga lugha
ashu-ashara/kumi
Mifano
Jisikia sukari
kuringa
Kaa ngumu
kutotishika/kuvumilia
Chongoa mtu
mfanyia mzaha
Kula njaro
kupuuza kazi
Piga nduthe
kimbia/toroka
Piga ngeta
kukaba koo
Leta diambo
zozana/lalamika
Ingia baridi
kuogopa
Pewa msomo
gombezwa
Kusota
kuishiwa na pesa
Ingia mitini
toweka/toroka
Kung`ara
kuvaa vizuri
Marehemu George
nguo za mitumba
Vaa chupa
vaa suruari nyembamba
Kujisikia poa
kuwa na furaha
Kula hepi
kuburudika
Lala kibahasha
tulia tuli baada ya kushindwa katika jambo
Sifa
Ni kauli fupi.
Hutumiwa na kundi dogo la watu.
Huzuka katika mazingira na kipindi maalum.
Ni lugha ya kimafumbo.
Hutumiwa na kundi dogo la watu katika jamii.
Huzuka na kutoweka baada ya muda.
Kunazo hudumu na kukubaliwa kama lugha sanifu k.v. matatu, bodaboda, chai, chokora, daladala, n.k.
Huwa na maana nyingi k.m. ‘mahewa’ humaanisha mziki, uongo au ulevi wa dawa za kulevya.
Maneno yana maana tofauti na ya kawaida.
Si lugha sanifu na hivyo haipaswi kutumiwa katika mazungumzo rasmi.
Hupendeza miongoni mwa watumizi.
Hutoweka baada ya matumizi kwa muda.
Hubadilika k.m. mbuyu na buda humaanisha baba.
Umuhimu
Kuficha siri ya wanaoitumia.
Kupanua lugha kimsamiati ikikubalika.
Kurahisisha mawasiliano kwa kuondoa uchovu wa urasmi.
Kuonyesha ubingwa wa lugha kwa kuhisi huonyesha umaarufu wa lugha
Kutenga wasio wana kikundi.
Kutafsidi/kupunguza ukali wa maneno k.m. Amepata bol-mimba.
Kupamba lugha na kuifanya ivutie
Kufanya wanakikundi wajihisi kuwa pamoja.
Kujitambulisha na watu wa kikundi fulani.
Shirikina
Semi ambazo huonyesha imani fulani ya kundi ya watu
Mifano
Ukijikuna kiganja cha mikono utapata pesa.
Ukila chakula gizani utakula na shetani.
Kuzaliwa ukiwa na vidole sita ni kuwa na bahati.
Bundi akilia karibu na nyumba mtu mmoja wa nyumba ile atafariki.
Umuhimu
Kukataza maovu.
Kuhifadhi utamaduni.
Kuchangia umoja wa kitaifa kwa aina moja ya itikadi kupatikana katika jamii nyingi.
Kutujulisha kuhusu itikadi za watu.
Tanakali za Sauti (Onomatopeya)
Maneno ambayo huiga sauti ya jambo, tendo au tukio fulani
Mifano
Boboka bobobo!
payuka ovyo ovyo
Bwakia bwaku
akia upesi upesi
Bwatika bwata
enda chini kwa mshindo
Bweka bwebwebwe!
lia kama mbwa
Chaga ngungundu
shikilia jambo
Ng’o!
kutoambulia chochote
Legalega lege
kosa kuwa imara
Chakua nyakunyaku
tafuna kwa kutoa sauti ya kuudhi
Bingirika bingiribingiri!
pinduka
Birua biru!
angusha na kupindua
Shindilia ndi!
Mianguko
Pu/kacha
tawi
Pu, pu, pu
mfululizo
Pukupuku!
mvua
Pwa!
kwa matope
Pwata!
kitu kinene
Tang’!
sarafu pagumu
Tapwi
matopeni
Tifu
mchangani
Tubwi/ chubwi
majini
Sifa
Ni kauli fupi.
Ni miigo ya sauti zinazotokea baada ya tendo fulani.
Hazina muundo maalum.
Hujumuishwa katika fani nyingine.
Hutumia takriri.
Umuhimu
Kuwezesha kuunda taswira ya jinsi mambo yanavyotokea.
Kuonyesha hisia fulani.
Kuongeza uzito kwa maneno.
Kuongeza utamu katika mazungumzo.
Kusisitiza jambo.
Kuipa lugha ladha na mvuto.
Kujenga tabia ya kusikiliza kwa makini ili kutambua mlio.
Kukuza ustadi wa kuiga na kuigiza.
Ni mbinu mojawapo ya mawasiliano.
Takriri za maana
Mafungu ya maneno yanayosisitiza na kueleza maana zaidi ya kitendo.
Mifano
Haambiliki hasemezeki
Siku nenda siku rudi
Tilia huku ukitolea kule
Hasikii la mwadhini wala la mteka maji msikitini
Umuhimu
Kutia ladha katika lugha na kuifanya iwe na mnato.
Kusisitiza jambo.
Kuonyesha ukwasi wa lugha ya mnenaji.
Tashbihi
Misemo ya ulinganisho
Sifa
Ni fupi.
Hutumia viungio kama, mithili ya, n.k.
Huwa na ujumbe wa kina.
Hutoa taswira ambayo husaidia keleza hulka kikamilifu.
Umuhimu
Kueleza sifa za kinazozungumziwa
Kuongeza lugha utamu
Kuonyesha umilisi wa lugha wa mtumizi
USHAIRI
Utanzu wa fasihi unaotumia lugha ya mkato inayoeleza maudhui yake kwa ufupi.
Sifa
Hutumia lugha ya kimkato.
Huwasilishwa mbele ya hadhira.
Huwasilishwa na mtu mmoja au kundi la watu.
Huwa na muundo maalum k.v. beti, vipande na vina.
Hutegemea sauti iliyo kipengele muhimu.
Huandamana na ishara za mikono, uso n.k.
Una mpangilio maalum wa maneno.
Una uteuzi maalum wa maneno.
Uwasilishaji wake huandamana na vitendo/uigizaji.
Hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa mdomo.
Huandamana na shughuli maalum k.v. matanga, kazi, n.k.
Huwa na mapigo ya kimziki au huweza kuimbika.
Huweza kuambatana na ala za mziki.
Hadhira hushiriki katika uwasilishaji wa ushairi simulizi.
Majukumu
Kuburudisha watu katika sherehe au shughuli fulani ya kijamii.
Kutakasa hisia au kutoa hisia zinazomsumbua mtu.
Kufunza maadili au tabia zinazokubalika na jamii.
Kufariji watu kutokana na maafa, kifo au kushindwa.
Kukuza uzalendo kwa kuhimiza watu kuiga waliotendea jamii mambo makuu k.v. mashujaa.
Kuhifadhi historia ya jamii k.m. maghani simulizi na tenzi.
Kuhifadhi na kudumisha utamaduni wa jamii.
Kuelimisha kuhusu suala fulani.
Kukashifu/kukejeli sifa mbaya za wabaya.
Kukuza umoja na ushirikiano katika jamii kwa kujumuisha watu pamoja.
Kusifu na kutukuza mashujaa katika jamii (tenzi).
Kukanya/kutahadharisha dhidi ya matendo maovu.
Kukuza urembo au usanii wa lugha kwa kuwa una ufundi mkubwa wa matumizi ya lugha.
Kuhamasisha jamii k.v. kisiasa.
Kukuza ubunifu kwa mtunzi na mwasilishaji
Kukuza ubunifu kwa kutunga kwa kuzingatia beti, mizani, vina na uteuzi maalum wa maneno.
Vipera vya Ushairi
wimbo
maghani
mashairi mepesi (utungo unaokaririwa)
ngojera (kwa majibizano)
tendi au rara (husimuliwa kwa mapigo ya kishairi)
Wimbo
Uungo wenye mahadhi ya kupanda na kushuka
Sifa
Huwasilishwa kwa njia ya mdomo.
Hutolewa kwa mahadhi ya kupanda na kushuka kwa sauti.
Hutumia lugha ya mkato.
Hadhira yaweza kuwepo au isiwepo.
Huwa na mwimbaji au waimbaji wanaoimba.
Waimbaji wanaweza kujivika maleba.
Huweza kuambatana na ala k.v. ngoma, zeze, kayamba n.k.
Huwa na urudiaji wa mstari au kifungu.
Aghalabu huimbwa na kupokezanwa baina ya kiongozi na waimbaji
Huimbwa tu au huambatana na kucheza.
Huweza kuandamana na shughuli fulani k.v. arusi, kazi, matanga, n.k.
Huwa na muundo maalum wa beti, mistari, vina, k.
Majukumu
Kuburudisha k.m. tumbuizo.
Nyenzo ya kiuchumi kwa baadhi ya watu.
Kuliwaza k.m. mbolezi.
Kuhimiza watu wakiwa kazini k.m. hodiya.
Kuelimisha kuhusu suala fulani k.m. ukimwi, ufisadi, n.k.
Kuhimiza uzalendo k.m. za siasa na taifa.
Kumbembeleza mtoto aache kulia au alale k.m. bembelezi.
Hadithi fupi na nyepesi za kishairi zenye visa vya kusisimua.
Mfano
Alichukua mkoba wake
Akanipa kisogo
Kana kwamba hakunijua
Kana kwamba hakusema, “Hadi mauko”.
Hakujali penzi letu
Hakujali wana
Ambao ndiye alowapa uhai
Alijua nilimpenda
Ila hata hilo alijipa kujipurukusha
Akayoyomea
Akamezwa na ulimwengu.
Sifa
Huhusu mambo ya kubuni au ya kweli k.v. sherehe ya uhuru, kesi ya mauaji, n.k.
Huhusu maswala ibuka na ya kawaida.
Hadithi huwasilishwa katika beti.
Huandamana na ala za mziki.
Hutolewa kwa toni ya kitanzia.
Huwa na visa vya kusisimua.
Huwa na ucheshi wenye kinaya.
Maswala hayatoleai kwa uwazi bali hufumbwa na kudokezwa.
Huwa na uigizaji/utendaji.
Mambo yanayosimuliwa hupigwa chuku.
Rara nafsi
Ushairi ambao hutungwa na mtu kuelezea hisia, matatizo na fikra zake mwenyewe.
Mfano
Muda umefika wa pingu kutiwa
Kutiwa silisili, kwani si utashi wangu
Ukoo waniuza, mithili ya kondoo sokoni
Mwambieni shangazi kwaheri nampigia
Hata angataka kuniopoa hawezi
Kwani mahari imetolewa
Mifugo kikwi nduguye amepokea
Kwaheri mama, kwaheri dada.
Sifa
Hugusia maswala yanayoathiri hisia za mtu binafsi kama vile mapenzi, usaliti, talaka, kifo.
Huwasilishwa kwa njia ya uimbaji unaoandamana na ala ya mziki.
Mzungumzaji huzungumza moja kwa moja na hadhira au aliyeandikiwa rara hii-mkewe, mpenziwe, mwanawe, Mungu, miungu.
Hutolewa katika miktadha k.v. mazishi kusifu aliyekufa, harusi na Bi. Arusi kama ameshinikizwa kuolewa.
Ngonjera
Mashairi ya kujibizana/kulumbana-yenye muundo wa kimazungumzo.
Sifa
Huwa na wahusika wawili au zaidi.
Mhusika mmoja huuliza jambo na mwingine hujibu.
Huendelezwa kwa njia ya wimbo.
Wahusika kupingana mwanzoni.
Wahusika huafikiana kufikiwa mwisho.
Umuhimu
Majibizano hukuza ubunifu kwa kila mmoja kuonyesha umaarufu.
Kukuza ujasiri wa kuzungumza hadharani.
Kuimarisha stadi ya kuongea.
Kuburudisha hadhira.
Mashairi Mepesi.
Mashairi ya kawaida ambayo hupatikana katika ushairi simulizi.
Hujumuisha mashairi mafupi ya kihisia, kimapenzi, kusifu na kukosoa watu.
Vigezo vya Uchanganuzi wa Tungo za Ushairi Simulizi
Kuainisha utungo kimaudhui/aina
Kuthibitisha ni aina fulani ya utungo wa kishairi/sifa.
Kutaja sifa zinazojitokeza za ushairi simulizi/utungo fulani wa ushairi simulizi.
Muktadha ambamo unaweza kutolewa.
Kuandika mbinu za kifasihi zilizotumiwa katika utungo huo.
Kufafanua sifa za jamii zinazojitokeza katika utungo.
Kuandika majukumu ya aina hiyo ya utungo wa ushairi katika
Anayeimba/nafsi imbi ni nani?
Kuandika maadili yanayojitokeza katika utungo.
Kueleza toni ya utungo huo.
MAZUNGUMZO
Maongezi ya mdomo yenye usanii.
Sifa
Huwa maongezi yenye usanii mkubwa.
Hutolewa mbele ya hadhira.
Hutolewa mbele ya hadhira.
Hutolewa kwa njia isiyokera.
Huambatana na sherehe fulani k.m. taabili katika matanga.
Hutegemea sauti na vitendo.
Huhusisha matumizi ya ishara k.v. za uso, mikono na miondoko.
Huhitaji ustadi wa kuzungumza ili kuteka hadhira.
Hutolewa na watu wenye umilisi mkubwa wa lugha.
Vipera vya Mazungumzo
Hotuba
Maelezo yanayotolewa mbele ya watu kuhusu mada fulani.
Huhusisha mada maalum sio suala lolote tu.
Umuhimu
Kuelimisha kwa kupa maarifa ya kukabiliana na maisha k.v. jandoni na arusini.
Kuadilisha au kutoa nasaha hadharani.
Huimarisha ukakamavu wa kuzungumza kadiri watu wanavyotoa hotuba hadharani.
Kukuza ufasaha na umilisi wa lugha.
Kupalilia kipawa cha uongozi.
Kuelimisha kwa kupatia watu maarifa ya kukabiliana na changamoto za maisha.
Aina za Hotuba
Risala
Hotuba inayowasilishwa mbele ya watu kueleza jambo fulani k.m. ya wafanyakazi kwa waajiri wao.
Mhadhara
Hotuba inayotolewa kwa hadhira fulani kufafanua somo au mada fulani.
Kumbukizi
Hotuba zinazohusu tukio fulani la kihistoria kuhusu mtu au kitu.
Mahubiri
Hotuba zinazohusu masuala ya kidini.
Taabili
Hotuba kuhusu aliyeaga dunia zinazohusu sifa zake nzuri.
Malumbano Ya Utani
Mazungumzo ya kutaniana.
Aina
Utani wa mawifi na mashemeji
Utani wa marafiki
Utani wa vijana
Utani wa watoto
Utani wa marika/ watu wa hirimu moja
Wewe ni mweusi kiasi kwamba ukiingia chumbani taa zinazimika.
Utani wa mababu/mabibi na wajukuu
Ee mume wangu, mbona walala mapema hivi? Utawezaje kulilinda boma letu ikiwa wewe ndiwe wa kwanza kujizika kitandani.
Utani wa maumbu (ndugu na dada)
Wewe unajifanya jasiri na juzi baba alikukemea kidogo tu ukaanza kutetemeka kama kondoo aliyenyeshewa.
Utani wa mazishi
Afadhali umekufa tukakuzika, sasa maghala yetu yatasalimika.
Utani wa makabila/ki ukoo
Wakikuyu wanapenda pesa kiasi kwamba maiti ikisikia mlio wa sarafu inaweza kufufuka.
Wakamba wa ukoo wa Akanga wanapenda nyama kiasi cha kula kijusi cha mbuzi.
Sifa
Huwa kati ya watu wawili au makundi mawili ya watu.
Hufanywa kwa kujibizana papo hapo.
Hufanywa kwa njia isiyo ya kuudhi.
Hutumia maneno ya mizaha.
Hutumia lugha ya ucheshi.
Hufanywa na watu wenye uhusiano mzuri.
Huchukua njia ya ushindani kila mmoja akitaka kumpiku mwenzake.
Watanianao huwa wamekubaliana kufanya hivyo.
Hufanyika katika wakati unaofaa sio baada ya kukutana tu.
Huhusisha masimango au kumkumbusha mtu wema uliomtendea.
Hutumia chuku sana kusisitiza au kukejeli sifa fulani hasi.
Huhusisha wakati mwingine utaniaji wa wasiokuwepo ukiambatanishwa na uigizaji wa kuchekesha.
Hutegemea uhusiano ulio kati ya wanajamii au makabila.
Huandamana na sherehe kama matanga.
Umuhimu
Kuburudisha kutokana na ucheshi.
Kuimarisha urafiki wa watu walio na uhusiano mwema wanaotaniana.
Hustawisha ufundi wa lugha.
Kukashifu tabia hasi k.v. ulafi, uchoyo, wivu, n.k.
Kukosoa wanajamii kwa njia ya kejeli/dhihaka
Kuimarisha umoja na ushirikiano kati ya wahusika.
Kuliwaza k.m. unaofanywa wakati wa maombolezo.
Kukuza na kudumisha mila na desturi za jamii.
Kukuza utangamano baina ya watu na wanajamii wanapokuja pamoja na kutaniana.
Kuhimiza watu kujieleza kwa uwazi kwa kupunguza urasmi miongoni mwa wanajaii.
Hudhihirisha uhusiano mwema baina ya watu wa jamii fulani.
Changamoto Sasa
Mabadiliko katika jamii yaliyosababisha baadhi ya wanajamii kupoteza nyenzo hii.
Kuingiliana kwa watu wa jamii mbalimbali.
Soga
Mazungumzo ya kupitisha wakati yasiyozingatia mada maalum.
Sifa
Hutokea baina ya watu wa rika moja.
Humithilisha uhalisia badala ya kuunakili.
Hutumia chuku na kufanywa ljambo lionekane kama halina uhalisia.
Hukejeli watu au hali fulani.
Wahusika ni wa kubuni.
Hutumia vichekesho kupunguza ukali wa ukweli uliomo.
Wahusika hupewa majina ya wanajamii husika.
Huwa na mafunzo au maadili.
Umuhimu
Kuburudisha kwa kuchekesha.
Kufunza maadili.
Kukejeli matendo yasiyofaa katika jamii
Kukuza ubunifu baina ya washiriki.
Kufunza kuhusu matendo na tabia za kibinadamu.
Huwa msingi wa utani unaokuwapo katika jamii.
Kuonya na kutahadharisha dhidi ya tabia siyokubalika.
Mawaidha
Mazungumzo ya kutoa ushauri kuhusu jambo fulani.
Sifa
Huwasilishwa mbele ya watu.
Hugusia takriban vipengele vyote vya maisha ya binadamu.
Aghalabu hutolewa na watu wenye umri mkubwa.
Hulenga maudhui maalum na ya aina nyingi kutegemea jinsia, umri, shughuli, n.k.
Hutumia lugha ya kubembeleza na isiyoonyesha ukali.
Hutumia lugha ya kuathiri hisia.
Huwa na ufasaha mkubwa wa lugha.
Ni mawazo mazito kuhusu maisha.
Hutolewa katika miktadha rasmi na isiyo rasmi.
Ujumbe hulenga hadhira maalum k.m. ya kike au kiume.
Hutumia fani nyingine za fasihi kama methali, misemo, ngano, nyimbo n.k. kupitisha mawaidha.
Huibua maadili yanayohitaji kuzingatiwa.
Muundo wa Mawaidha
Utangulizi
Kutoa kauli ya kuvutia makini ya hadhira k.v. ‘Utu uzima huenda na uwajibikaji’, au kueleza kiini cha mawaidha.
Mwili
Kutoa wosia, maonyo, maelekezo kutegemea suala analotolea mawaidha akitumia jazanda, kupanda na kushuka kwa sauti, kimya, miondoko, kubadilisha kasi ya kuzungumza, kudondoa semi za watu maarufu, n.k.
Hitimisho
Kuonyesha msimamo kuhusiana na suala analozungumzia.
Kushirikisha hadhira ili kujua msimamo wao kuhusu suala alilowausia.
Hadhira kutoa changamoto kuhusiana na mawaidha yanayotolewa.
Umuhimu wa mawaidha
Kuelekeza jamii kimaadili.
Kuelekeza kuhusu jinsi ya kukabiliana na changa moto maishani.
Kushauri jinsi ya kutenda jambo fulani.
Kujasirisha waoga na kuwapa ukakamavu.
Kuwaondolea wanajamii ujinga.
Kuhifadhi na kuendeleza mila na desturi za jamii.
Njia ya kipato kwa baadhi ya watu.
Kuelimisha kuhusu maarifa ya kuendeshea maisha, majukumu na matarajio ya jamii.
Ulumbi
Uwezo na ustadi wa kuzungumza kwa uhodari mkubwa.
Miktadha Ambamo Ulumbi Hutumika Katika Jamii
katika mijadala mbungeni
katika hotuba za kisiasa
katika mahubiri maabadini
katika mijadala shuleni
kortini
katika shughuli za kijamii k.v. posa
katika sala/dua
katika maapizo
katika malumbano ya utani
katika majigambo/vivugo
Sifa
Hufanywa mbele ya hadhira.
Huwa na lengo maalum k.v. kushawishi, kuelimisha, kushauri n.k.
Hutumia tamathali za usemi kwa ufanifu mkubwa k.v. chuku, misemo, methali, n.k.
Lugha huwa yenye mvuto na ufasaha.
Hutumia lugha yenye taharuki na ushawishi.
Unenaji huambatana na utumizi wa ishara/ viziada lugha.
Uwasilishaji huwa sahili na wenye ujumbe mzito.
Huwa na urudiaji mwingi ili kusisitiza na kuvutia usikivu.
Huwa na matumizi ya taharuki k.v. mtuo.
Huwa na mtiririko mzuri wa mawazo.
Sifa za Mlumbi
Asiwe mwoga ili kuweza kuzungumza hadharani.
Asiwe na haya ili kuweza kuzungumzia mambo ya aibu inapobidi.
Awe mchanganfu na mcheshi ili kunasa makini ya hadhira na kuzuia isikinai.
Awe na ufahamu mpana wa utamaduni wa hadhira asitumie maneno na ishara zinazoweza kuwaudhi au kupingana na imani za hadhira.
Awe na uwezo wa kuingiliana vizuri na hadhira ili aivutie.
Awe na kumbukumbu nzuri ili ulumbi wake utiririke vizuri.
Awe na uwezo wa kudramatisha ili kuonyesha picha fulani k.v. ishara za uso, mwili, miondoko kuonyesha picha ya analozungumzia.
Awe na ujuzi na ufasaha wa lugha ili kuwasilisha mawazo kwa njia mwafaka na inayovutia.
Aweze kubadilisha toni na kiimbo hadhira isikinai.
Awe na uwezo wa kushirikisha hadhira k.v. kwa maswali ya balagha ili kuondoa uchovu wa kusikiliza.
Awe na uwezo wa kutumia mtuo wa kidrama ili kuongeza taharuki, kusisitiza ujumbe na kuteka makini ya hadhira.
Umuhimu
Hukuza uwezo wa kujieleza na kusema hadharani kwa kujiboresha kadiri anavyoendelea.
Kigezo cha kuteulia viongozi wa baadaye kwani ushawishi humtambulisha mlumbi kama mwenye uwezo wa kuongoza.
Kuelimisha jamii kwa njia isiyochosha.
Kudumisha umoja na ushirikiano jamii inapokusanyika pamoja kusikilizaulumbi.
Kuhamasisha na kuzindua jamii juu ya suala fulani.
Kushawishi walengwa wakubali jambo fulani.
Kukuza uwezo wa mwanajamii kushawishi na kupatanisha.
Kushawishi watu wapende jambo fulani.
Kuburudisha wasililizaji.
Maapizo
Maombi maalum ya kumtaka Mungu, miungu au mizimu kumwadhibu mhusika hasidi, mkinzani au muovu.
Mfano
Ikiwa kweli wewe ni mkazamwanangu,
Nami ndiye nilompa uhai mwana unoringia,
Anokufanya upite ukinitemea mate,
Chakula kuninyima, wajukuu kunikataza ushirika,
Miungu nawaone chozi langu, wasikie kilio changu,
Mizimu nawaone uchungu wangu,
Radhi zao wasiwahi kukupa,
Laana wakumiminie,
Uje kulizwa mara mia na wanao,
Usiwahi kufurahia hata siku moja pato lao,
Watalokupa likuletee simanzi badala ya furaha,
Wakazawanao wasikuuguze katika utu uzima wako!
Sifa
Yalitolewa kwa waliokwenda kinyume na matarajio ya jamii.
Yalifanywa mahali maalum k.v. makaburini, porini, chini ya miti mikubwa, n.k.
Hutolewa kwa ulaji kiapo.
Yalitolewa na mwathiriwa au watu maalum walioteuliwa.
Maapizo huaminiwa yataleta maafa kwa jamii.
Watoaji maapizo walikuwa walumbi.
Maapizo hutumia lugha kali inayonuiwa kutia woga ili kutahadharisha dhidi ya maovu.
Umuhimu
Kuonya na kutahadharisha wanajamii dhidi ya maovu.
Kutambulisha jamii kwani kila mojawapo ina aina yake ya kuapiza.
Kukuza umoja katika jamii kwani kaida na miiko hufanya wanajamii kujihisi kuwa kitu kimoja.
Kuadilisha wanajamii kwa kujifunza kutenda mema ili kuepuka laana.
MAIGIZO
Utanzu wa fasihi simulizi unaoambatana na vitendo.
Kuonya na kutahadharisha watu dhidi ya kufaya mambo yasiyofaa.
Kuelimisha watu wafahamu jambo fulani k.v. ukimwi, ufisadi, n.k.
Kukosoa watu wanaofanya kinyume na matarajio ya jamii k.v. wivu, uchoyo, n.k.
Kupitisha maarifa na amali za kijamii.
Ploti
Utangulizi-kutambulisha mgogoro
Ukuzaji wa mgogoro
Kilele cha mgogoro
Usuluhishaji wa mgogoro
Aina za maigizo
Maigizo Ya Kawaida
Maonyesho ya jadi yakiwa yameondolewa kwenye mazingira yake halisi.
Sanaa ya Maonyesho
Matendo ya kweli yanayojitokeza katika jamii kulingana na mazingira yake halisi k.m. uganga, mazishi, unyago, ngoma, n.k.
Tofauti
Maigizo ya kawaida
Sanaa ya maonyesho
ü Mazingira ya kuzua/maalum
ü Matukio ya kuiga
ü Huwa na wahusika na hadhira maalum
ü Matumizi ya ukumbi na jukwaa maalum
ü Hutumia maleba na vifaa vya kuzua mazingira maalum
ü Hugawika katika maonyesho Kutumia lugha kwa njia maalum
ü Wahusika hufanya mazoezi kabla ya igizo halisi
ü Hutumia mazingira halisi
ü Matukio halisi/ ya kila siku.
ü Washiriki na waigizaji walio pia hadhira
ü akuna haja ya ukumbi wala jukwaa
ü Hakuna vifaa maalum bali huwa mazingira yenyewe.
ü Muundo wake hufululuza au hayajagawika katika maonyesho.
ü Hawahitaji kufanya mazoezi kwani ni matukio ya kila siku.
Maigizo ya kawaida
Michezo ya Kuigiza
Maigizo ambayo huwasilishwa na watendaji jukwaani mbele ya watu.
Sifa za Mwigizaji bora
Awe jasiri ili aweze kuigiza mbele ya watu/hadharani.
Awe na ubunifu ili aweze kufanya uigizaji kuvutia na kuondoa ukinaifu.
Awe na ujuzi wa kutumia ishara za uso, mwili na miondoko kuonyesha picha ya hali anayoigiza.
Awe na ujuzi na ufasaha wa lugha ili kuwasilisha mawazo kwa njia mwafaka na inayovutia.
Aweze kubadilisha toni na kiimbo kulingana na hali tofauti anazoigiza k.v. huzuni.
Awe na uwezo wa kushirikisha hadhira kwa maswali ya balagha ili kuondoa uchovu.
Awe na uwezo wa ufaraguzi/ kubadilisha uigizaji wake papo hapo kutegemea hadhira yake na kutoa mifano inayofahamika kutoka katika mazingira ya hadhira.
Awe anaelewa utamaduni wa hadhira yake ili asitumie maneno na ishara ambazo zinaudhi ama kukinzana na na imani zao.
Vichekesho
Michezo ya kuigiza inayokusudiwa kuzua kicheko ili kupitisha ujumbe k.m. vioja, vitimbi n.k.
Sifa
Vichekesho huigizwa.
Huwasilishwa kwa lugha sahili.
Hujaa taswira zinazoweza kutambulika na hadhira.
Hutumia mbinu ya kejeli, kunaya na tashtiti.
Vichekesho huwa vifupi.
Havihitaji uchambuzi wa ndani ili kuvielewa au kupata maana.
Jukumu
Kuburudisha hadhira kwa kuchekesha.
Kuelimisha kwa kuonyesha jambo la kijinga alilofanya mtu.
Njia ya kuwapatia watu riziki.
Hutumika katika hadithi kuifanya ivutie.
Kukejeli kitendo fulani kisichofaa alichofanya mtu fulani.
Kukashifu matendo hasi ya kijinga.
Kuadilisha ama kutoa funzo fulani la tabia njema.
Ngonjera
Ngonjera inayoambatana na uigizaji/utendaji.
Sifa
Kuweko kwa uigizaji/utendaji k.v. ishara za uso na mikono.
Huwa na wahusika wawili au zaidi.
Huendelezwa kwa njia ya wimbo.
Mhusika mmoja huuliza jambo na mwingine hujibu.
Wahusika kupingana mwanzoni.
Wahusika hufikia uafikiano kufikia mwisho.
Michezo ya Watoto/Chekechea
Michezo inayoigizwa na watoto katika shughuli zao.
Aina
Mchezo wa baba na mama
Kuruka kamba
Kujificha na kutafutana
Kukimbiza kibaramwezi dhidi ya upepo ili kizunguke
Mchezo wa baba na mama
Sifa
Waigizaji ni watoto.
Huhusu shughuli za kiuchumi na kitamaduni k.v. arusi, siasa, ukulima.
Huandamana na nyimbo za watoto.
Huwa na miondoko mingi k.v. kujificha, kuruka.
Huwa na matumizi mengi ya takriri.
Huchezwa popote.
Huwa na kanuni fulani.
Hukoma watoto wakichoka au wakikiuka kanuni
Umuhimu
Kufunza watoto majukumu yao ya utu uzima.
Kuwatanguliza watoto katika sanaa ya uigizaji.
Kukuza ubunifu wa watoto kadiri wanapoendelea kuigiza.
Kudumisha utamaduni wa jamii.
Kuburudisha watoto.
Kukuza stadi ya uigizaji miongoni mwa watoto.
Kukuza utangamano miongoni mwa watoto kwa kuwajumuisha pamoja.
Kukashifu matendo hasi ya watu wazima kwa watoto.
Kuwapa watoto ukakamavu na kujiamini wakiwa wachanga.
Majigambo/vivugo
Uigizaji ambapo wahusika hujigamba kwa matendo ya kishujaa.
Mfano
Ndimi Kisoi, dume la ukoo mtukufu
Ulojipamba kwa mabingwa
Wachezaji hodari wa ngoma
Ndimi dume liloingia nyanjani
Makoo yakatetemeka
Yakang’ang’ania, ngozi kusakata nani
Kijiji kizima kilinijua
Wazee walilienzi
Wakamiminika kiamboni
Mabinti kunikabithi.
Sifa
Aghalabu huambatana na ngoma.
Hujitokeza, kujigamba na kisha kuendelea kucheza ngoma.
Anayejigamba hubeba zana zake za vita kama vile mkuki na ngao kuonyesha aliyotenda.
Anayejigamba huvaa maleba kuambatana na jambo analojisifia.
Utambaji
Usimulizi wa hadithi unaoambatana na uigizaji.
Huwa na matumizi ya vizuizui.
Mazingira
Uigizaji wa maumbile asilia yaliyozunguka jamii ya watu k.v. sauti za wanyama.
Kuna matumizi ya viziuzui, matawi n.k.
Sanaa ya Maonyesho
Ngoma
Uchezeshaji wa viungo vya mwili kuambatana na mdundo au miondoko maalum.
Aina
Ngoma za wanawake
Ngoma za tohara
Ngoma za wanaume
Ngoma za sherehe
Ngoma za vijana
Ngoma za unyago na jando
Ngoma za wazee
Ngoma za arusi
Ngoma za kufukuza mapepo
Ngoma za kuaga mwaka
Sifa
Huandamana na muziki na ala ya muziki k.v. ngoma.
Ngoma huchezewa mahali wazi na penye hadhira.
Wachezaji huvaa maleba maalum kulingana na funzo linalonuiwa.
Huwa na wahusika aina mbili; watendaji na watazamaji kwa wakati mmoja.
Huweza kuandamana au kutoandamana na sherehe.
Hutofautiana kulingana na jamii husika.
Umuhimu
Kuburudisha kwa ufundi wa kucheza kwa kuzingatia miondoko.
Kitambulisho cha jamii kwani kila moja ina aina yake ya ngoma.
Kuhifadhi na kuendeleza tamaduni za jamii husika.
Kukuza uzalendo kwa kuwafanya wanajamii kuionea fahari jamii yao.
Kukuza umoja na ushirikiano kwa kujumuisha watu pamoja.
Kuelimisha kwa kupitisha mafunzo na maarifa.
Matambiko
Utoaji wa kafara kwa Mungu, miungu, pepo au mizimu ili wasaidiwe kutatua shida, kutoa shukrani au kuomba radhi.